SWAHILI TRANSLATIONS

by Kades

Below are two poems amongst the forty two ANNO’S POEMS that I have managed to translate to Swahili. Once am convinced that they sound well and am sure they depict what Anno had in mind I will send them through. Personally I think they sound well and I will want to read them in my own language once am through. Am hopeful it will be a good Swahili book. Am sorry for the delay but I try to write when my mind is free en pure from anything so that I can create the right picture.



JARIBIO LA KUPUMUA/TRYING TO FIND AIR

Who Said the Race Is Over?
page 12
Translated at 9.31 pm on 29/03/2007

Napata katika jina lako, maneno ya mombi.
Kwa kukumbatia, Napata pa kuweka majibu.
Katika kizuka chako,Napata yakinisho la miaka,
Na vile nilivyo hoi.

Na katika ujana.

Nikijaribu kupunga hewa katika masaa yapingayo uwepo wako.

Naelezewa kuwa nimebarikiwa,
kwa rehani ya busara uliyoniwekea-
Ilinigharimu amani yangu.
Naota sasa na wezi wa benki,
Naota na makaa, na asubuhi za majira ya baridi…
Naota juu ya kupoteza maisha yangu.

Na hizi ndizo ndoto zangu zitishazo.
Hakuna malaika tena, upindi wa mvua wala mabawa.


HOFU YA MAKOSA/TERROR OF MISTAKES

Who Said the Race Is Over? page 24
Translated at 8:04 pm on 29/10/2008

Tu wadhaifu
na twahitaji ibada.
Dalili za kweli wangu uhapa kama damu-
Katika kuta zako,
Katika ulimwengu wako
Kioo chako.

Je ni mimi nikoseae katika mawazo yangu?
Haupaswi kukosoa njia zangu nzuri-
Kwa kuwa mimi ni ujana!

Ukweli hauna sauti kuu,
milele sio jasiri na haujali zaidi ya sasa.
Na hofu ya kukosa katu sio kuu.

Lakini sisi sio wadhaifu sana.

Tuna nguvu zaidi tukiwa tumeunganishwa na ngoma,
Na tunapumua kuambatana na mlio wake.
Na joto la jua linatuweka matumaini.